Jumanne 8 Julai 2025 - 21:56
Taarifa ya Walimu 102 wa Masomo ya wazi na Masomo ya Kiwango cha Juu wa Hawza ya Qom, kwa ajili ya kumuunga mkono Imam Khamenei

Hawza/ Kundi la walimu wa masomo ya wazi na ngazi za juu katika Hawza ya Qom wametangaza kwamba: Kwa kufuata na kuiga Marjaa wakubwa wa Taqlid na walimu wetu mashuhuri, tunatangaza kuwa tutalijibu kwa kutoa roho zetu na pumzi zetu na katika uwanja wa jihadi kubwa, shambulizi lolote la kudhalilisha au kuivunjia heshima sehem tukufu ya Imam wa Ummah.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, matini kamili ya taarifa ya walimu 102 wa masomo ya juu ya wazi na ngazi za juu wa Hawza ya Qom ni kama ifuatavyo:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu

Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, Mola wa walimwengu, na rehma zimshukie Muhammad na kizazi chake watoharifu, na laana ya Mwenyezi Mungu iwe juu ya maadui wao hadi Siku ya Malipo.

Kwa heshima ya walimu wakubwa mashuhuri Mwenyezi Mungu awalinde

Kwa kuwasalimu kwa heshima na kwa kutoa rambirambi zetu kutokana na mnasaba wa siku za huzuni kwa watu wa Mwenyezi Mungu, pamoja na kupata shahada baadhi ya wapiganaji, wanazuoni na wananchi wapenzi:

Jamhuri Tukufu ya Kiislamu ya Iran, ambayo imewasilisha mbele ya mataifa mfano wa moja kwa moja wa mtazamo wa Fiqhi ya Kishia kuhusu kusimamisha Kitabu cha Mwenyezi Mungu na yale yaliyoteremshwa, imeweza kufafanua mahali pa makutano kati ya maisha ya kidini yanayofaa na uja wa Mwenyezi Mungu pamoja na kunufaika na neema za kimada, na katika njia hii ya fahari imefanikiwa kufikia hatua ya maendeleo ya kielimu ya kisasa, teknolojia za kisasa na kupanua ustawi wa kijamii na kiuchumi katika kivuli cha uadilifu, kupitia kuimarisha miundombinu ya msingi ya maendeleo ya kimada – licha ya mapungufu na makosa ya baadhi ya watendaji wake – kiasi kwamba maendeleo hayo yamekuwa hali halisi isiyokanushika, licha ya uadui, upotoshaji wa vyombo vya habari na ushawishi wa kimtazamo wa kipropaganda, na hatimaye mfumo wa kibeberu umelazimika kuungana ili kuzuia maendeleo haya na kulazimika hata kushiriki moja kwa moja kijeshi dhidi ya maarifa ya msingi ya maendeleo ndani ya Iran.

Hata hivyo, Jamhuri ya Kiislamu ambayo Imam mwasisi wake aliyekuwa mtukufu aliijenga tangu "siku ya kwanza" juu ya msingi wa ucha Mungu na radhi za Mwenyezi Mungu, leo hii imefikia kiwango cha ustawi na utukufu mbele ya muungano wa matwaghuti na nguvu za kibeberu kiasi kwamba kwa kutegemea ahadi za kweli za Mwenyezi Mungu, na kukabiliana na  maadui duniani kote, imesimama kama kiongozi wa Ummah wa Kiislamu na kinara wa harakati ya muqawama wa Kiislamu duniani, na kwa niaba ya wapenda uhuru na wanyonge wote wa dunia, wakati ambapo usiku mmoja, kwa dhana batili ya adui Mzayuni, mfumo wake wa kijeshi ulionekana kuwa umeteketezwa, lakini kwa kutegemea wilaya ya Mwenyezi Mungu ya kifiqih, iliweza kutoa shambulio zito na kali zaidi katika historia dhidi ya utawala wa Kizayuni katika ardhi zilizoporwa ndani ya muda wa saa chache tu. Na katika kivuli cha bendera ya Kiislamu inayopaa, Iran imekuwa nchi pekee duniani ambayo asubuhi humpiga mawe shetani wa Kizayuni na usiku humpiga mawe shetani wa Kimarekani, na kwa njia hii Hija ya mwaka huu ya Waislamu imekamilika kwa kupiga mawe mashetani wa kikanda na kimataifa.

Katika ushindi huu mkubwa, ambao majeshi ya haki na Hizbullah wameupata katika zama za ghaiba kubwa ya Imam wa Zama – arwāḥunā lahul fidā’ – chini ya uongozi waliyu faqih mkubwa na kiongozi mkuu wa Kishia, Ayatollah al-‘Uẓmā Sayyid Ali Khamenei – dāma dhilluh – msururu wa mapigo makali kutoka kwa fikra ya damu ya fiqhi ya Kishia kuanzia hukumu za jihadi hadi Mapinduzi ya Kiislamu yenye fahari, umeshambulia kwa nguvu mfumo wa kitwaghuti, wa kibeberu na majeshi ya Iblisi, hadi kufikia kiwango cha uwezo na ukali kiasi kwamba vita ya leo dhidi ya Israel imekuwa vita ya Uislamu wote dhidi ya ukafiri wote, na ushindi huu ni mkono wa Mwenyezi Mungu – "yadullāh" – wa Amīrul-Mu’minīn, ambao baada ya karne nyingi umetokeza tena kupitia mwanawe, na unaivunja heshima ya ukafiri kwa daraja iliyo bora zaidi ya ibada za viumbe wawili (binadamu na majini).

Katika hali hii, adui dhaifu na mnyonge ambaye ameshangazwa mno na mashambulizi makali ya Iran, hakupata njia nyingine ila kutoa vitisho dhidi ya nguzo kuu ya hema la ushindi la Jamhuri ya Kiislamu – yaani uwepo wa kimungu wa Ayatollah al-‘Uẓmā Sayyid Ali Khamenei – dāma dhilluhul-‘ālī – bila kujua kuwa hilo ni utangulizi wa pigo lingine kali kutoka kwa viongozi na mafaqihi wa hawza dhidi ya mwili dhaifu wa kitwaghuti.

Uwepo wa kimakini na wa kuelimisha wa walimu mashuhuri baada ya maneno ya Marjaa wakubwa wa Taqlid kwa ajili ya kumtetea Imam wa Ummah wa Kiislamu katika zama za ghaiba, umeufanya ulimwengu wa matwaghuti kuonja ladha ya uchungu, na umeifanya harufu ya kupendeza ya utii kwa Uislamu na Ahlulbayt (as), pamoja na wanyonge duniani na wote walioungana na uongozi wa kimungu, kuenea kila mahali.

Japokuwa hali hii ya upeo wa maarifa na utambuzi wa wakati ni jambo linalotegemewa kutoka kwa nafasi tukufu ya fiqhi na elimu, hata hivyo, tunatoa shukrani zetu kwa unyenyekevu kwa hatua yenu hii ya stahiki, yenye athari, na ya kimujahidina, na tunatangaza – kwa kufuata na kuiga Marjaa wakubwa wa Taqlid na walimu wetu mashuhuri – kuwa tutalijibu kwa kutoa roho zetu na pumzi zetu na katika uwanja wa jihadi kubwa, shambulizi lolote la kuidhalilisha au kuivunjia heshima ya sehemu tukufu ya Imam wa Ummah.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu ampe maisha marefu yenye afya salama, heshima na mamlaka, kiongozi mkuu na kiongozi wa Waislamu – Ayatollah al-‘Uẓmā Sayyid Ali Khamenei – dāmat barakātuh – chini ya uangalizi wa Imam wa Zama (arwāḥunā lahul fidā’), na awape maisha marefu yenye baraka Marjaa wa ngazi ya juu na walimu mashuhuri, pamoja na kuipa Jamhuri Tukufu ya Kiislamu ushindi na ukuu zaidi na zaidi.

"Na wale waliodhulumu watakuja kujua ni upande gani wataugeukia"

Imesainiwa na kundi la walimu wa ngazi za juu na masomo ya wazi wa Hawza ya Qom.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha